Wilaya za Algeria
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wilaya za Algeria ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi nchini Algeria. Tangu tarehe 18 Desemba 2019, nchi imegawanywa katika sehemu 58 zinazoitwa wilaya. Zinafanana zaidi na mikoa ya Tanzania. Wilaya hizo 58 imegawanywa katika baladiyah 1,541 ( tarafa). Jina la wilaya daima ni lile la mji mkuu wake.
Kwa mujibu wa katiba ya Algeria, wilaya zimekabidhiwa madaraka kadhaa. Kila wilaya huwa na bunge lake la kieneo ambalo linaitwa Assemblée Populaire Wilayale kwa Kifaransa au المجلس الشعبي الولائي al-majlis al-sha'abi al-wila'i kwa Kiarabu.
Mkuu wa serikali ya wilaya huteuliwa na rais wa jamhuri akiwa na cheo cha "wali". Bunge la wilaya huwa na madaraka kuhusu makisio yake. Mapato yake ni idadi ya kodi za kieneo pamoja na ruzuku kutoka serikali kuu.[1]
Bunge la Wilaya lina mamlaka fulani kuhusu maswala ya afya, ustawi wa jamii, utalii, shule, michezo, mipango ya miji na ujenzi wa makazi, kilimo, maji na misitu, miundombinu wa kieneo, urithi wa kiutamaduni, na maswala ya maendeleo ya kieneo kwa jumla.
Remove ads
Orodha
Hadi mwaka1984 idadi ya wilaya za Algeria ilikuwa 48. Mnamo 2019, wilaya 10 mpya ziliongezwa. [2] [3]
Remove ads
Tangu 2019
Tarehe 26 Novemba 2019, Baraza la Mawaziri la Algeria lilipitisha sheria ya kuongeza tena majimbo 10, kwa kugawa baadhi ya majimbo makubwa kusini mwa Algeria. [4] Kwa hivyo, mikoa ifuatayo imeongezwa mnamo Desemba 18, 2019:
- Mkoa wa Bordj Badji Mokhtar
- Katika Jimbo la Salah
- Mkoa wa Djanet
- Katika Mkoa wa Guezam
- Mkoa wa El M'Ghair
- Mkoa wa Toggourt
- Mkoa wa Béni Abbes
- Mkoa wa Timimoun
- Mkoa wa Ouled Djellal
- Mkoa wa El Menia
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads