Rabanus Maurus
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Rabanus Maurus Magnentius (Mainz, 780 hivi – Oestrich-Winkel, 4 Februari 856), alikuwa mmonaki Mbenedikto maarufu kama mwanateolojia na mhubiri, ambaye akawa askofu mkuu wa Mainz, Ujerumani.

Ndiye mtunzi wa kamusi elezo De rerum naturis ("Mambo ya uasilia") na wa vitabu mbalimbali kuhusu malezi, sarufi na ufafanuzi wa Biblia[1].
Kwa umuhimu wake kati ya walimu wa kipindi cha Karolo Mkuu, aliitwa "Praeceptor Germaniae" ("mwalimu wa Ujerumani").
Anasifiwa kwa kutoacha chochote alichoweza kufanya kwa utukufu wa Mungu [2].
Katika Martyrologium Romanum anatajwa kama mtakatifu wa Kanisa Katoliki, sikukuu yake ikiwa tarehe 4 Februari[3].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads