Retisi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Retisi (pia: Reticius, Rheticius, Rheticus, Rhétice; alifariki 320 hivi) kwa miaka 25 hivi alikuwa askofu wa Autun, leo nchini Ufaransa, akiwa wa kwanza kati ya wanaojulikana [1][2].
Kwa agizo la kaisari Konstantino Mkuu alishiriki sinodi mbili zilizojaribu kumaliza farakano la Donato lilitokea Afrika Kaskazini[3].
Gregori wa Tours alimsifu katika maandishi yake [3] na Jeromu alimtaja pamoja na vitabu viwili alivyoviandika[4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads