Rio Negro (Amazon)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Rio Negro ni mto ambao unapitia msitu wa mvua wa Amazonas katika kaskazini-magharibi ya Brazil, kwenye jimbo la Amazonas.

Unaitwa Negro (Kihispania na Kireno kwa "nyeusi") kwa sababu maji yake yanabeba vyembe vya ardhi ambavyo hufanya maji yaonekane kama chai. [1] [2] Ni mto mkubwa wa maji meusi duniani.
Rio Negro ndiye tawimto kubwa zaidi la mto Amazonas upande wa kushoto (kadiri inavyoelekea bahari). Huanza huko Kolombia na kuishia kwenye Amazonas.
Rio Negro ina utajiri mkubwa wa spishi tofauti. Karibu aina 700 za samaki zimeorodheshwa katika beseni la mto, na imekadiriwa kuna jumla ya spishi 800- 900 za samaki. [3] Kati ya hizo ni nyingi ambazo ni muhimu katika biashara ya samaki wa kufuga nyumbani.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads