Venezuela

From Wikipedia, the free encyclopedia

Venezuela
Remove ads

Venezuela ni nchi kaskazini mwa Amerika ya Kusini.

Ukweli wa haraka
Remove ads


Thumb
Ramani ya Venezuela.

Imepakana na Brazil, Guyana na Kolombia.

Mbele ya pwani ya Bahari ya Karibi kuna madola ya visiwani ya Aruba, Antili za Kiholanzi na Trinidad na Tobago.

Venezuela ilikuwa koloni la Hispania hadi mwaka 1811 na lugha ya Kihispania ni lugha ya kitaifa.

Kikatiba Venezuela ni shirikisho la jamhuri.

Mji mkuu ni Caracas.

Remove ads

Asili ya jina "Venezuela"

Jina la nchi ni umbo la Kihispania la jina la mji wa Venezia (Italia). Amerigo Vespucci, mpelelezi Mwitalia katika utumishi wa mfalme wa Hispania, aliona vijiji vya wenyeji waliojenga nyumba juu ya maboriti yaliyosimamishwa katikati ya maji karibu na mwambao pasipo kina. Vijiji vilimkubusha mji wa Venezia uliojengwa vilevile. Venezuela yamaanisha "Venezia Ndogo" katika Kihispania.

Jiografia

Thumb
Nyumba ya "palafito" jinsi ilivyoonekana zamani za Amerigo Vespucci.

Venezuela ina eneo la km² 916,445 (kama Namibia) ikiwa na pwani yenye urefu wa km 2,800. Asilimia 39 za eneo hili ni misitu, mashamba ya kulimwa ni 4%, eneo la mifugo 20%, mazao ya kudumu kama kahawa 1%.

Kuna kanda nne za kijiografia:

Milima ya meza

Nyanda za juu za Guayana zina milima ya pekee: kuna milima ya meza 115 inayoitwa "tepui" katika lugha ya wakazi asilia. Kiekolojia hilo ni eneo muhimu kwa sababu milima mingi ina mimea na wanyama wa pekee, tofauti na milima jirani, na inapatikana hapa tu kote duniani.

Maporomoko marefu duniani yatelemka kutoka milima hii kama vile maporomoko ya Salto del Angel ("anguko la malaika") ambako maji huanguka mita 965.

Mito

Mto mkubwa wa Venezuela ni Orinoco wenye urefu wa km 2574 unaoishia katika Atlantiki. Lakini mkono wa Brazo Casiquiare unajitenga na kuishia katika mto wa Amazonas nchini Brazil.

Matawimto muhimu ya Orinoco ni Rio Apure na Rio Caroni.

Majimbo katika shirikisho

Tazama pia Majimbo ya Venezuela
Thumb
Mlima wa meza Mt. Roraima
Thumb
Los Barrios ni mitaa ya vibanda vya Caracas


Venezuela ni shirikisho la madola au majimbo 23 ya kujitawala, maeneo yasiyojitawala na mkoa wa shirikisho wa Caracas.

Maelezo zaidi Jimbo, Mji Mkuu ...
Remove ads

Watu

Wakazi wengi (51.6%) wanajiainisha kama machotara wa Kizungu-Kiindio. Wazungu ni 43.6%, wenye asili ya Afrika ni 3.5% na Waindio 2.6%. Utafiti wa DNA unaonyesha kwamba urithi wa jeni kwa asilimia 60.6 ni wa Kizungu, 23 ni wa Kiindio na 16.3 ni wa Kiafrika.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania, ingawa lugha asilia zinakubalika kwa Waindio, na lugha nyingine zinatumiwa na wahamiaji.

Upande wa dini, 88% ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (71%) na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (17%).

Tazama pia

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela

Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Venezuela kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads