Rudolf Sherwin
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Rudolf Sherwin (Rodsley, Derbyshire, 25 Oktoba, 1550 – Tyburn, 1 Desemba 1581) alikuwa padri wa Uingereza maarufu kwa akili na imani[1].

Mwaka mmoja baada ya kupata digrii ya pili aliacha ushirika wa Anglikana ili kujiunga na Kanisa Katoliki, alipata upadrisho huko Ufaransa mwaka 1577, alikwenda Roma alikokaa miaka 3[2], halafu akatumwa kwao alipofanya utume kwa siri miezi michache tu[3].
Alipokuwa gerezani mwaka mzima aliongoa wengi na hatimaye alinyongwa na kukatwa vipandevipande. Maneno yake ya mwisho yalikuwa: "Iesu, Iesu, Iesu, esto mihi Iesus!"[4].
Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius IX mwaka 1929 na mtakatifu mwaka 1976 na Papa Paulo VI.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 1 Desemba[5].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads