Rugaruga
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Rugaruga ilikuwa jina kwa aina mbalimbali ya askari wa kienyeji katika Afrika ya Mashariki wakati wa karne ya 19 na 20.

Remove ads
Rugaruga wa Mirambo
Jina "Rugaruga" lilikuwa maarufu tangu miaka ya 1860 kama jina la askari wa Mtemi Mirambo aliyekuwa mtemi wa Wanyamwezi katika magharibi ya Tanzania ya leo.
Mirambo aliwahi kutajirika kama mfanyabiashara kwa njia ya misafara kati ya pwani ya Bahari Hindi na Kongo. Alitumia sehemu kubwa ya utajiri wake kujenga jeshi la binafsi. Kwa kusudi hii alinunua bunduki aina ya magobori na kukusanya vijana wengi walioitwa "rugaruga". Kwa kawaida vijana hao walikuwa wanaume walioishi bila ukoo na bila familia waliowahi kutoroka kwenye hali ya utumwa au kuwa wapagaji wa misafara.[1] Mirambo aliwapokea na kuwapa silaha na kwa njia hii alishinda maadui hadi kuwa mtemi mkuu wa Waynamwezi kuanzia 1860 hadi kifo chake mnamo 1884. Rugaruga hawa walihofiwa kote na Mirambo aliweza kupanusha eneo lake kwa msaada wao. Inasemekana ya kwamba kabla ya mapigano walipewa pombe na banghi kwa kusudi ya kuongeza ukali na kupunguza hofu yao ya kifo.
Remove ads
Rugaruga kama wanajeshi wa kienyeji
Kutokana na askari wa Mirambo jina la "Rugaruga" lilijulikana kote likawa kawaida kwa askari wa watawala wengi. Wajerumani walipotwaa eneo la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani walikuta neno hili mahali pengi lilikuwa njia ya kutaja askari au mapolisi wa kienyeji.[2]
Wakati wa ukoloni ilikuwa pia jina la wasaidizi waliotolewa na vijiji au machifu kwa msaada wa jeshi rasmi la koloni. Kwa mfano wakati wa vita ya maji maji vikosi wa jeshi la kikoloni viliongezeka vikundi vya "rugaruga" walioteuliwa na machifu kuwasaidia kukandamiza upinzani wa maji maji. Wale rugaruga walikuwa tofauti na askari Waafrika ndani ya jeshi la kikoloni waliovaa sare rasmi wakiteuliwa na kufundishwa kufuatana na utaratibu wa Kijerumani.[3] Kwa maana hii rugaruga walipatikana upande wa Wajerumani na pia upande wa Waingereza huko kenya.
Remove ads
Polisi wa machifu wakati wa koloni
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia neno "rugaruga" ilikuwa jina la mapolisi na askari waliokuwa wasaidizi wa machifu ndani ya utawala wa kikoloni wa Kiingereza nchini Tanganyika na Kenya.[4]
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads