S2Kizzy

Producer S2KIZZY From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Salmin Kasimu Maengo (maarufu kwa jina lake la kisanii S2KIZZY, amezaliwa 9 Mei 1996) ni mtayarishaji wa muziki na mtunzi wa nyimbo kutoka Tanzania. Anafahamika zaidi kwa kutengeneza nyimbo za Bongo Flava “Amaboko” na “Tetema” za Rayvanny akimshirikisha Diamond platnumz. Ametayarisha albamu  na kusimamia kazi za Diamond Platnumz, Rayvanny, Bill Nass na Vanessa Mdee. Anasifiwa kuwa 'mtayarishaji bora' katika muziki wa kisasa wa Bongo-Flava, Bongo-Trap, Afrobeats na Afro-pop.[1]

Remove ads

Kazi

Maengo ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Pluto Records, lakini anafanya kazi hasa na WCB (Wasafi Classic Baby).[2]

Huenda Amber Rose anafanya naye kazi kwenye mradi. [3]

Maisha ya awali na mwanzo wa kazi

Salmin, aliyepewa jina la Rais wa Zanzibar Marehemu Salmin Amour, alizaliwa Mbeya, na kulelewa na shangazi yake kama wake. Mama yake alifariki akiwa na umri wa miaka 3, muda mfupi baada ya hapo baba yake aliondoka na kuoa tena. Alilelewa katika maadili ya Kiislamu.

Shauku yake ya muziki ilianza mapema, na akiwa shule ya msingi alianza kujifunza jinsi ya kupiga ngoma. Baadaye, akiwa sekondari alisoma shule ya bweni ya kwiro boys iliyopo Morogoro, Tanzania.

Remove ads

Marèjeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads