Rayvanny
Mwanamuziki na mtunzi wa nyimbo wa Tanzania kutoka WCB Wasafi Record label From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Raymond Shaban Mwakyusa (anafahamika zaidi kwa jina lake kama Rayvanny; amezaliwa tarehe 22 Agosti mwaka 1993) ni mwimbaji na mtunzi wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania (kwa asili ni mtu wa mkoani Mbeya).
Remove ads
Wasifu
Rayvanny alianza kujulikana kupitia wimbo wake wa Kwetu, na si muda mrefu baada ya hapo, Harmonize alitolea wimbo wake wa Bado. Baadaye, Rayvanny alitoa Natafuta Kiki na Sugu, ambazo ni nyimbo zilizotolewa kama ziada, hasa ukizingatia kuwa Sugu ilitumia biti ya wimbo wa Bow Wow uitwao What's My Name. Mambo yaliendelea na kuja wimbo Mbeleko, Shikwambi, Zezeta, na Kijuso, aliyoimba na Queen Darleen. Alitolewa pia Pochi Nene, aliyoimba na S2kizzy, na baadaye wimbo Mwanza, alioimba na msanii mwenzake Diamond Platnumz.
Hata hivyo, wimbo Mwanza ulifungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutokana na kukosa maadili mema, jambo lililosababisha kutofanya vizuri kwenye vyombo vya habari nchini Tanzania.
Baada ya Mwanza kufungiwa, Rayvanny na Diamond walitolea wimbo Tetema, ambao ulipendwa na watu wengi na kufanikiwa kuwa na watazamaji wengi kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mfupi sana. Alikuwa chini ya lebo ya WCB Wasafi inayomilikiwa na Diamond Platnumz, ambako alishirikiana na wasanii kama Harmonize na Diamond mwenyewe. - Baadaye alianzisha lebo yake binafsi iitwayo Next Level Music ,akionyesha dhamira ya kukuza vipaji vipya na kujitegemea kisanii.
Remove ads
Albamu
[[The Big One ni mojawapo ya kazi zake kubwa, ikichanganya mitindo mbalimbali kama Afrobeat, hip-hop, R&B, na gospel. - Nyimbo maarufu: Kwetu, Tetema (aliyoshirikiana na Diamond), Number One, Natafuta Kiki, Sugu, na Wasi Wasi.
Ushirikiano
Rayvanny amefanya kazi na wasanii wakubwa wa Afrika kama: - [[Diamond Platnumz - Harmonize - Alikiba]] - Mwamposa (katika nyimbo zenye ujumbe wa kiroho)
Mafanikio
- Ameshinda tuzo mbalimbali za muziki ndani na nje ya Tanzania. - Amekuwa mfano wa mafanikio kwa vijana wengi wanaotamani kuingia kwenye muziki wa kizazi kipya. Rayvanny ametoa nyimbo mpya kali mwaka 2025 kama “I Miss You” na “Zuena”, huku lebo yake ya Next Level Music ikiendelea kukuza vipaji vipya tangu alipoianzisha mwaka 2021 baada ya kuondoka WCB Wasafi.
Nyimbo Mpya za Rayvanny (2025)
Rayvanny ameendelea kuwa moto wa kuotea mbali katika muziki wa Bongo Flava na Amapiano. Hizi ni baadhi ya nyimbo zake mpya za 2025: - “I Miss You” ft. Zuchu – Wimbo wa mapenzi uliotayarishwa na Sound Boy - “Stay” ft. Abby Chams – Mchanganyiko wa R&B na Afrobeat - “Rara” – Umetayarishwa na Lizer, una ladha ya Amapiano - “Zuena” ft. Mbosso & Weasel – Wimbo wa kimapenzi wenye mguso wa Afrika Mashariki - “Baila” – Wimbo wa dansi wenye midundo ya Sound Boy - “Nitongoze (Amapiano Remix)” – Toleo jipya la Amapiano - “Twerk It” ft. Musa Keys – Ushirikiano wa kimataifa - “Maisha Amapiano” ft. DJ Tarico – Ujumbe wa maisha kwa ladha ya kusisimua - “Amapiano Freestyle 2025” – Onyesho la ubunifu wake binafsi
Remove ads
Historia ya Next Level Music (NLM)
- Ilianzishwa: Mwaka 2021 na Rayvanny baada ya kuondoka rasmi WCB Wasafi mwezi Julai 2022 - Makao makuu: Dar es Salaam, Tanzania - Lengo kuu: Kukuza vipaji vipya vya muziki wa Afrika Mashariki na kuendeleza uhuru wa kisanii - Wasanii waliowahi kusainiwa: Mac Voice, Jay Melody (kwa ushirikiano), na wengine chipukizi - Uzalishaji: NLM imehusika katika kutengeneza nyimbo na video zenye ubora wa kimataifa
Remove ads
Tuzo
Rayvanny akiwa chini ya NLM aliendelea kushinda tuzo kubwa na kutumbuiza kimataifa, ikiwemo MTV EMA 2021
Rayvanny pia ametoa albamu kama Sound From Africa (2021) na EPs kama Flowers, New Chui, na Flowers II, ambazo zimechangia kukuza jina lake kimataifa.
Albamu
Nyimbo za Rayvanny 2021
- "Number One" (Remix) ft. Zuchu
- "Koroga" ft. Kizz Daniel
- "Mama"
- "Lala" ft. Jux
- "Sweet" ft. Guchi
- "Prison"
- "Baila"
- "Falling in Love"
- "Nyamaza"
Rayvanny pia 2021 alizindua albamu yake ya SOUND FROM AFRIKA, ambayo ilikuwa na nyimbo nyingi zinazoshirikisha wasanii wa kimataifa kama Kizz Daniel, Zlatan, Nasty C, na wengineo.
Nyimbo za Rayvanny 2022
- "Te Quiero" ft. Marioo
- "Mbele Kwa Mbele" ft. Young Lunya
- "Mon Amor" ft. Mbosso
- "Nitongoze" ft. Diamond Platnumz
- "I Miss You" ft. Zuchu
- "Vacation"
- "Kilio" ft. Phina
- "Forever"
2023 Katika mwaka wa 2023, Rayvanny alitoa nyimbo kadhaa zilizopata umaarufu mkubwa katika tasnia ya muziki wa Bongo Flava. Baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na:
"Nitongoze" akishirikiana na Diamond Platnumz. Wimbo huu ulipokelewa vyema na mashabiki na ulijumuishwa katika orodha ya nyimbo bora za Bongo Flava za mwaka 2023.
"Mwambieni" akimshirikisha Macvoice. Wimbo huu ulitolewa chini ya lebo ya Next Level Music na ulipata umaarufu mkubwa.
"Forever". Huu ni wimbo wa mapenzi ambao ulitolewa rasmi na video yake kupatikana kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki.
"Down". Wimbo huu ulitolewa na video yake rasmi ilipokelewa vizuri na mashabiki.
"Christmas". Wimbo huu ulitolewa wakati wa msimu wa Krismasi na ulilenga kusherehekea sikukuu hiyo.
2024 Katika mwaka wa 2024, Rayvanny ametoa nyimbo kadhaa mpya ambazo zimepata umaarufu mkubwa. Baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na:
- "Nesa Nesa" akishirikiana na Diamond Platnumz na Khalil Harrison.
- "Angelina" akimshirikisha King Promise.
- "Peponi" akiwa na DJ Davizo.
- "Wow" akishirikiana na Otile Brown.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads