Saidi Ntibazonkiza
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Saidi Ntibazonkiza (alizaliwa Bujumbura, 1 Mei 1987) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka Burundi anayechezea klabu ya Simba S.C. ya Tanzania na timu ya taifa ya Burundi.
Remove ads
Kucheza mpira katika ujana wake
Katika ujana wake alichezea klabu ya Vital'o, bingwa wa Burundi. Alichezea timu ya taifa ya umri wa vijana na pia alicheza mechi 7 za timu kuu ya taifa.
Kwenda kwake Uholanzi
Alikuja Uholanzi mwaka 2005 kwa njia ya kuomba kimbilio la hifadhi ya kisiasa. Klabu ya NEC ilimchunguza na kuona kuwa ni mchezaji ambaye atafaa katika mustakabali kwa hiyo ikamchukua. Kutokana na umri wake mdogo klabu ikamweka katika kikosi cha NEC ya vijana ili kufanya mazoezi na vijana. Kocha wa timu kuu ya NEC, Mario Been, baada ya kuona mchezaji huyo ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo akaona amweke katika timu kuu inayoshiriki katika Ligi Kuu ya Uholanzi. Basi, kijana huyo amecheza mechi nyingi katika Ligi kuu hiyo pakiwemo mechi dhidi ya Ajax Amsterdam na Feyenoord Rotterdam na timu nyingine mashuhuri na alionekana katika mechi hizo kuwa ni mchezaji mzuri.
Remove ads
Kuweka mkataba na NEC
Mchezaji huyo aliweka mkataba na klabu hiyo, mkataba utakwisha mwaka 2009.
Katika mechi yake ya kwanza aliyoicheza katika kombe la UEFA Cup dhidi ya FC Dinamo Bucuresti alionekana mchezaji mzuri kabisa na alipata zawadi ya mchezaji bora katika mechi hiyo, na kwa sasa mchezaji huyo anacheza dakika zote bila kugombolewa na amekua kiungo muhimu zaidi katika klabu yake kwa sasa.
Januari mwaka 2009 aliweka mkataba wakuongeza myaka, ongeza yake hiyo ilimfanya abaki kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2012 [1]
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads