Samsoni

From Wikipedia, the free encyclopedia

Samsoni
Remove ads

Samsoni (kwa Kiebrania שִׁמְשׁוֹן, Shimshon, Šimšôn, "Mtu wa jua"[1]) alikuwa mmojawapo kati ya Waamuzi wa Biblia.

Thumb
Samson akipigana na simba kadiri ya Lucas Cranach the Elder, 1525.
Thumb
Samsoni kipofu kadiri ya Lovis Corinth, 1912.

Kadiri ya Waamuzi 13-16 alikuwa wa kabila la Dan, alizaliwa na mwanamke tasa, akawa mnadhiri tangu achukuliwe mimba, akapewa nguvu ya ajabu kutokana na nadhiri hiyo, akapigana na Wafilisti hadi kifo chake alipowaua kwa pamoja wengi kuliko maisha yake yote[2].

Hadithi zake zinaonyesha kwamba alikuwa jitu lakini mwenye akili ya kitoto na tamaa nyingi ambazo hatimaye zilimponza.

Hata hivyo Waraka kwa Waebrania 11:32-34 unamsifu kwa imani yake iliyompa nguvu.

Remove ads

Tanbihi

Loading content...

Viungo vya nje

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads