Sanami

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Sanami anatajwa kati ya Wakristo wa kwanza kuuawa kwa ajili ya imani yake barani Afrika (180 hivi).

Ni kati ya wafiadini wa Madauros (karibu na M'Daourouch, leo nchini Algeria), pamoja na Namfamo, Mijin na Luchíta[1]. Majina mengine yanayotajwa pamoja ni: Adyuto, Aresto, Artifa, Besa, Datulo, Degno, Evasi, Felisi, Felisiani, Kresto, Kwarti, Kwinti, Lukania, Martiri, Mose, Museo, Onorato, Orato, Paulo, Pompini, Privati, Reduktula, Rogasiani, Rustiko, Salvatori, Saturnini, Setimini, Sesiliana, Seliani, Sidini, Simplisi, Sito, Teturo, Tino, Vikta, Viktorino, Vikturi na Vinsenti.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu kadiri ya barua ya Masimo wa Madaura kwa Augustino wa Hippo.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 18 Desemba[2][3].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads