Sauti Sol
Bendi ya afro-pop ya Kenya iliundwa Nairobi From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sauti Sol ni bendi ya afro-pop ya Kenya iliyoanzishwa mjini Nairobi, [1] Kenya, na waimbaji Bien-Aimé Baraza, Willis Chimano na Savara Mudigi mwaka wa 2005. [2] [3] [4] Hapo awali kilikua kikundi cha cappella, mpiga gitaa Polycarp Otieno alijiunga kabla ya kujiita Sauti Sol. [5]
Sauti Sol walitoa albamu yao ya kwanza ya studio, Mwanzo, tarehe 1 Novemba 2008, na kupata sifa kubwa kutoka kwa wakosoaji. Albamu yao ya pili ya studio, Sol Filosofia, ilitolewa tarehe 25 Februari 2011, na kuwapa kundi hilo tuzo na uteuzi kadhaa katika mchakato huo. Tarehe 18 Juni 2012, bendi hiyo ilitoa albamu ya muda mfupi kwa kushirikiana na rapa na mtayarishaji wa rekodi kutoka Afrika Kusini, Spoek Mathambo. [6]Albamu yao ya tatu ya studio, Live and Die in Afrika, ilitolewa mtandaoni tarehe 21 Novemba 2015.[7]
Bendi hiyo imefanya ziara kadhaa zilizofanikiwa barani Afrika na Ulaya, ikiongoza chati za muziki nchini Kenya na kupata umaarufu wa kimataifa kupitia maonyesho barani Ulaya na Marekani, pamoja na kuonekana kwenye televisheni na kupata tuzo na uteuzi mbalimbali. Hii ni pamoja na onyesho lao la tamasha la mwaka 2011 nchini Kenya na kundi la a cappella kutoka Afrika Kusini, Ladysmith Black Mambazo. Bendi hiyo pia imepokea tuzo na uteuzi wa ndani na wa kimataifa, ikiwemo kwenye Kisima Music Awards[8], Channel O Music Video Awards[9], MTV Europe Music Awards[10], na BET Awards.[11]
Remove ads
Washiriki wa bendi
- Bien-Aimé Baraza – Mtunzi wa nyimbo, Gitaa, Piano.
- Willis Chimano – Mwimbaji, Mwigizaji, mpiga Keytar.
- Savara Mudigi - Mwimbaji, Mtayarishaji, ngoma, gitaa la Bass.
- Polycarp Otieno – Mpiga Gitaa, Mtayarishaji, Mtunzi, Mpiga Gitaa.
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads