Segun Arinze

Muigizaji wa Nigeria From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Segun Arinze (Segun Padonou Aina; alizaliwa 1965 [1]) ni mwigizaji na mwimbaji wa Nigeria.[2][3][4][5][6]

Maisha ya awali na elimu

Segun alizaliwa Onitsha, jimbo la Anambra na baba wa kabila la Yoruba na mama wa kabila la Igbo. Ni mzaliwa wa Badagry, jimbo la Lagos. Alihudhuria Victory College of Commerce huko Ilorin, kisha akaenda Taba Commercial College iliyopo jimbo la Kaduna baada ya kumaliza elimu yake ya shule ya upili.

Alisomea Michezo ya Kuigiza katika Obafemi Awolowo University. Anafahamika almaarufu kama Black Arrow ambapo alipata jina hilo katika uhusika alioigiza.[7]

Alimuoa mwigizaji mwenzake wa Nollywood Anne Njemanze, ambae baadaye alikuja kuwa na maisha ya ndoa mafupi kuliko alioyaishi.[8] Wanandoa hao walikua na binti mmoja, Renny Morenike, aliyezaliwa tarehe 10 Mei.[9]

Remove ads

Kazi

Alianza uigizaji ndani ya Ilorin. Mbali na uigizaji, Segun pia ni mkufunzi wa waigizaji na kwa sasa anafanya kazi na African international film festival kwa kutoa maarifa kwa kizazi kijacho cha waigizaji.[10][11][12]

Filamu zilizochaguliwa

  • Women in Love
  • Anini
  • Darkest Night
  • Extra Time
  • Fragile Pain
  • Across the Niger
  • Church Business
  • To Love a Thief
  • Silent Night
  • Chronicles (with Onyeka Onwenu and Victor Osuagwu)
  • 30 Days
  • Family on Fire (2011)
  • A Place in the Stars (2014)
  • Invasion 1897 (2014)[13][14]
  • An eye for an eye
  • Deepest Cut (2018) - with Majid Michel and Zach Orji
  • The Island Movie (2018)
  • Gold Statue (2019)

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads