Sekondinus
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sekondinus ni mmoja wa mashahidi wa imani ya Kikristo waliouawa tarehe 7 Machi 203 mjini Karthago wakati wa dhuluma dhidi ya Wakristo chini ya serikali ya Kaisari Septimius Severus (193-211).

Anaheshimiwa tangu kale kati ya watakatifu wafiadini pamoja na watakatifu Perpetua na Felista wanaojulikana zaidi kama mashahidi Wakristo wa Afrika ya Kaskazini.
Pamoja na akina mama hao vijana na wanaume wengine 3 walikamatwa pamoja na kutupwa jela. Jinsi ilivyokuwa kawaida walipewa nafasi ya kuachana na Ukristo lakini wote walisimama imara wakabatizwa gerezani.
Walihukumiwa adhabu ya kifo katika uwanja wa michezo mbele ya watu wengi. Hukumu ilitekelezwa kwa njia ya wanyamapori. Waliraruliwa na wanyama mbalimbali, wakamalizwa kwa upanga, isipokuwa yeye aliyefariki gerezani [1].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads