Uwanja wa michezo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Uwanja wa michezo (Kilat. + Kiing. stadium) ni mahali pa mashindano ya michezo. Mara nyingi umezungukwa na majengo ambayo yanaweza kufunguliwa juu na kuwezesha umma kutazama onyesho hilo kwa kutumia nafasi za kusimama au kukaa. Viwanja mara nyingi hutumiwa pia kwa matamasha na mikutano ya hadhara.



Remove ads
Historia
Viwanja vya michezo vilipatikana tayari katika miji mingi ya Ugiriki ya Kale ambako mashindano yalitekelezwa kwa heshima ya miungu. Mashuhuri hasa vilikuwa viwanja vya Olimpia na Delfi[1].
Katika Roma ya Kale viwanja vilitumiwa hasa kwa matamasha ya mapigano na uwindaji. Mfano mashuhuri ni Koloseo wa Roma. Jengo hili lilikuwa kielelezo wa viwanja vingi vya kisasa.

Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads