Servulo wa Roma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Servulo wa Roma (alifariki Roma, Italia, 23 Desemba 590) alikuwa ombaomba jijini Roma aliyelala tangu utotoni mbele ya kanisa la Mt. Klementi kutokana na hali yake ya kupooza mwili mzima[1].

Pamoja na mateso yake hayo, aliishi kwa imani kubwa, akimshukuru Mungu na kuwagawia maskini wenzake alichopewa na wafadhili.
Papa Gregori I aliandika juu yake sura moja ya kitabu cha Majadiliano.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 23 Desemba[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads