Sevilla
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sevilla ni mji mkubwa kando ya mto Guadalquivir kusini mwa Hispania na mji mkuu wa jimbo la kujitawala la Andalusia.


Mwaka 2019 wakazi wake walikuwa 688,592 [1] na kuufanya wa nne nchini kwa wingi wa watu.
Historia
Mji ulianzishwa zamani za Wafinisia ukaja kukaliwa na kutawaliwa na Waroma wa Kale, Wavandali halafu na Wavisigothi na tangu mwaka 711 na Waarabu Waislamu. Mwaka 1248 ulitekwa na wafalme wa Kastilia na kubaki upande wa Hispania ya Kikristo.
Majengo mengi mazuri yanatunza kumbukumbu ya historia hiyo. Boma la Alcazar lilijengwa na mafundi Waislamu kwa niaba ya wafalme Wakatoliki. Sevilla ilikuwa na ofisi kuu ya utawala kwa makoloni ya Hispania katika Amerika.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads