Shazia Manzoor
Mwimbaji wa Pakistani From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Shazia Manzoor ni mwimbaji maarufu wa Pakistan.

Maisha ya awali na kazi
Shazia Manzoor alizaliwa Rawalpindi, Punjab, Pakistan. Alianza kuimba kwa kufanya onyesho katika maonyesho ya chuo Rawalpindi.[1] Shazia Manzoor alifunzwa muziki na Ustadhi Feroz wa Gwalior gharana.[2] Ni mwimbaji maarufu Pakistani na India, na miongoni mwa diaspora wa Punjabi. Shazia Manzoor anaimba sana sana muziki wa Kipunjab. Aliimba sana nyimbo tofauti tofauti za watu wa Punjab na mashairi ya Punjabi Sufi. Pia mara nyingine anaimba nyimbo za Kiurdu.
Remove ads
Nyimbo maarufu
Ni maarufu kwa nyimbo zake zifuatazo:
- Aaja Sohniya,
- Mahi Aavega
- Maye Ni Kinnu Akhan
- Chann Mere Makkhna
- Dhol Mahia
- Akh Da Nasha
Pia ametumbuiza katika matamasha ya upendo baada ya mafuriko ya Pakistani ya 2010 ili kutunisha mfuko kwa wahanga wa mafuriko. Shazia alitambulishwa mwaka 1992 na mchekeshaji, Umer Shareef, kama alivyosema katika mahojiano wakati wa kumshukuru Noor Jehan pamoja na Zille Huma.[3]
Alikuwa msanii mshirikishwaji katika Coke Studio (Pakistani) (awamu ya 8 2015). Ametumbuiza katika BBC Philharmonic Orchestra London.[4]
Remove ads
Albamu teule
- Raatan Kaaliyan (June 1998)
- Aarfana Kalaam (August 1999)
- Chan mere Makhna (December 2001)
- Hai Dil Jani (September 2003)
- Ishq Sohna (August 2009)
- Tu Badal Gaya (March 2010)
- Jatt London (February 2011)
- Balle Balle (May 2011)
- Sahib teri bandi haan (February 2012)
- Dhokebaaz (Chip Shop) (November 2012)
- Aish Karo (April 2015)
- ’’Akh Da Nasha’’ (August 2018)
- Burger & Chips Shop (July 2019)
Amepongezwa kwa onyesho lake ndani ya Coke Studio Msimu 8, Sehemu 6 kutokana na wimbo wa harusi wa Awadhi "Hare Hare Bans" pamoja na Ustadhi Rizwan na Ustad Muazzam.
Ushirikiano na wengine
- 1999: Dark And Dangerous (Pamoja na Bally Jagpal)
- 2001: Untruly Yours (Pamoja na Bally Jagpal)
- 2001: Vix It Up (Pamoja na DJ Vix)
- 2002: Dark And Direct (Pamoja Bally Jagpal)
- 2005: Groundshaker (Pamoja na Aman Hayer)
- 2009: Collaborations 2 (Pamoja na Sukshinder Shinda)
- 2014: 12B (Pamoja na Bally Jagpal)
- 2014: Collaborations 3 (Pamoja na Sukshinder)
- 2018: Akh Da Nasha (Zakir Amanat)
Uimbaji kwenye filamu
Shazia Manzoor pia ameimba (playback) kwenye filamu nyingi zikiwa pamoja na Pal Do Pal (1999 ) na Ishq Khuda (2013). Uimbaji wake kwenye filamu zilizofanikiwa kibiashara mwaka 2003 ulipongezwa sana na umma.[5]
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads