Sidoni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sidoni (kwa Kiarabu صيد, Ṣaydā, kwa Kigiriki Σιδών, Sidon) ni mji wa Lebanoni kusini, katikati ya Beirut na Tiro, maarufu katika historia ya kale hasa kwa utajiri uliotokana na biashara yake ya kupitia baharini. Hata leo unategemea sana bandari yake, mbali ya utalii.





Wakazi walikuwa 65,000 hivi mwaka 2000, lakini pamoja na eneo la kandokando wanafikia 200,000[1][2] na kuufanya mji wa tatu nchini Lebanoni.
Remove ads
Katika Biblia
Katika Biblia mji huo unatajwa mara nyingi, kuanzia Kitabu cha Mwanzo hadi Injili na Matendo ya Mitume.
Wengi kutoka maeneo yake walikwenda kumsikiliza Yesu (Mk 3:8; Lk 6:17), naye alitembelea maeneo yake (Mk 7:24; Math 15:21) na kusema ungetubu mapema kuliko Wayahudi wenzake aliowahubiria kwa kuwapa uthibitisho wa miujiza mingi (Math 11:21-23).
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads