Tiro

From Wikipedia, the free encyclopedia

Tiro
Remove ads

Tiro au Turo (kwa Kiarabu صور, Ṣūr, kwa Kigiriki Τύρος, Týros) ni mji wa Lebanoni kusini maarufu katika historia ya kale hasa kwa utajiri uliotokana na biashara yake ya kupitia baharini. Hata leo unategemea sana bandari yake.

Thumb
Bandari ya Tiro.
Thumb
Tao la Ushindi.
Thumb
Magofu ya kiwanja cha michezo Al Mina.
Thumb
Magofu ya jukwaa huko Al Mina
Thumb
Sehemu ya kusini ya mji wa leo.

Jina la mji linamaanisha "mwamba"[1] na kutokana na mwamba ambao mji umejengwa juu yake hapo awali.

Wakazi walikuwa 117,000 hivi mwaka 2003,[2][3] na kuufanya mji wa nne nchini Lebanoni.[4]

Utalii unavutiwa na magofu ya zamani, kikiwemo kiwanja cha mashindano ya mbio ya farasi cha wakati wa utawala wa Warumi kilichoorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia mwaka 1979.[5].

Remove ads

Katika Biblia

Katika Biblia mji huo unachukuliwa kama kielelezo cha kiburi; hata hivyo Yesu alisema ungetubu mapema kuliko Wayahudi wenzake aliowahubiria kwa kuwapa uthibitisho wa miujiza mingi (Math 11:21-23) na hata hivyo bado walionesha uzito (ugumu) wa kuamini na kumpokea.

Dondoo lenyewe ni hili: Mathayo 11:21 “Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.

22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.

23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo”.

Remove ads

Tanbihi

Loading content...

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads