Sila

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Sila au Siluano (kwa Kigiriki: Σίλας / Σιλουανός; karne ya 1 AD) ni mmojawapo kati ya viongozi muhimu zaidi wa Kanisa la mwanzo huko Yerusalemu[1].

Kutoka huko alitumwa mara nyingi kwa Wakristo wasio Wayahudi kushughulikia matatizo mbalimbali (kuanzia Mdo 15:22) akawa mwenzi wa Mtume Paulo katika safari za kimisionari (kuanzia Mdo 16:25) akatimiza hadi mwisho huduma zake kwa neema ya Mungu na bidii isiyokubali kuchoka.

Anatajwa na Paulo katika barua mbalimbali (k.mf. 2Kor 1:19).

Hatimaye alimsaidia Mtume Petro kuandika waraka yake wa kwanza (1 Pet 5:12).[2]

Anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu, ila tarehe ya sikukuu yake ni tofautofauti. Kwa Wakatoliki ni tarehe 13 Julai[3].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads