Simoni wa Crepy
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Simoni wa Crepy (au wa Vexin; Bar-sur-Aube, Ufaransa, 1048 hivi - Roma, Italia, 30 Septemba 1082) alikuwa mtawala wa Amiens, Vexin na Valois miaka 1074-1077.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 30 Septemba[1].
Maisha
Baada ya kuoa, alikubaliana na mke wake waachane na mali yao wakatawe monasterini. Hata hivyo, kwa kutoridhika na utajiri wa mazingira ya Condat, baadaye alikwenda kuishi upwekeni kwenye misitu ya Jura.
Kutoka huko aliitwa mara kadhaa kufanya upatanisho kati ya watawala waliopigana vita.
Pia alihiji hadi Nchi takatifu halafu Roma alipofariki huku akisaidiwa sakramenti za mwisho na Papa Gregori VII.
Alizikwa kwenye basilika la Mt. Petro[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads