Sumve
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sumve ni kata ya Wilaya ya Kwimba katika Mkoa wa Mwanza, Tanzania. Msimbo wa posta ni 33814.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 19,195 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 16,436 waishio humo.[2]
Jina linatokana na kijiji kimoja kiitwacho Sumve ambapo miaka mingi ya nyuma, kabla ya wamisionari kuanza kuishi katika kijiji, palikuwa na watu wafahamikao kama Wasomva. Hao walitokea maeneo ya Tabora na kazi yao ilikuwa kutengeneza majembe, mapanga na kuyauza, lakini baada ya wamisionari kuja wakayaacha maeneo hayo na kurudi kwao Tabora.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads