Mkoa wa Tabora

mkoa wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkoa wa Tabora
Remove ads

Mkoa wa Tabora ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Tabora ni jina la mji, wilaya na mkoa wa Tanzania ya kati. Eneo la mkoa ni kubwa kuliko ya mingine yote nchini, likiwa na Km² 76,151; km2 34,698 (46%) ni hifadhi ya misitu, km2 17,122 (22%) ni hifadhi ya wanyama. Mikoa inayopakana nalo ni: upande wa kaskazini Shinyanga, upande wa mashariki Singida, upande wa kusini Mbeya na Songwe, upande wa magharibi Katavi, Kigoma na Geita. Jumla ya wakazi ilikuwa watu 3,391,679 (2022[1]). Makao makuu yako Tabora Mjini.

Ukweli wa haraka Nchi, Wilaya ...
Thumb
Ramani ya Mkoa wa Tabora na wilaya zake 7.
Thumb
Tabora wakati wa ukoloni wa Wajerumani.

Msimbo wa posta ni namba 45000.

Remove ads

Wilaya na wakazi

Kuna wilaya 8 (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022[2]): Tabora Mjini (308,741), Nzega Vijijini (574,498), Nzega Mjini (125,193), Igunga (546,204), Uyui (562,588), Urambo (260,322), Sikonge (335,686), Kaliua (678,447). Jina la Urambo humkumbuka Mtemi Mirambo aliyekuwa mtawala muhimu wa Wanyamwezi kabla ya kuingia kwa ukoloni.

Wenyeji wa Tabora ni hasa Wanyamwezi. Walio wengi ni wakulima na wafugaji.

Remove ads

Usafiri

Mkoa wa Tabora una barabara za lami. Ipo inayoanzia Tabora mjini hadi Nzega kuelekea Mwanza, pia kutoka Nzega kuelekea Igunga mpaka Singida, nyingine ipo inayoanzia Tabora mjini mpaka Urambo yenye urefu wa km 93 na nyingine inaanzia Tabora mjini mpaka Manyoni yenye urefu wa km 254 ukipitia Itigi.

Kuna njia ya reli ya kati kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwa upande mmoja na kwenda Mwanza kwa upande mwingine.

Remove ads

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

  • Bukene : mbunge ni Suleiman Zedi (CCM)
  • Igalula : mbunge ni Ntimizi Rashidi Mussa (CCM))
  • Igunga : mbunge ni Dk. Dalaly Peter Kafumu (CCM)
  • Kaliua : mbunge ni Magdalena Sakaya (CUF)
  • Manonga : mbunge ni Seif Hamis Said Gulamali (CCM)
  • Nzega Mjini : mbunge ni Hussein Bashe (CCM)
  • Nzega Vijijini : mbunge ni Hamis Kigwangallah (CCM)
  • Sikonge : mbunge ni George Kakunda (CCM)
  • Tabora Mjini : mbunge ni Emmanuel Mwakasaka (CCM)
  • Ulyankulu : mbunge ni John Peter Kadutu (CCM)
  • Urambo : mbunge ni Margareth Sitta (CCM)
  • Uyui : mbunge ni Maige Athumani Almas (CCM)

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads