Suzana U Surim
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Suzana U Surim (1803 - Seoul, 20 Septemba 1846) ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.
Mjane huyo na wafiadini wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[1]
Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba[2].
Walionyongwa katika magereza mbalimbali siku moja naye ni: Laurenti Han Ihyong, Petro Nam Kyongmun, Yosefu Im Chipek, Teresa Kim Imi, Agata Yi Kannan na Katerina Chong Choryom[3].
Remove ads
Mazingira
Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu katika rasi ya Korea, nchi ya Kikonfusyo, kwa juhudi na ari za wananchi walei[4].
Mwaka 1836 Korea ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society) ambao walilisha na kuthibitisha imani kwa kutangaza Neno la Mungu na kuadhimisha sakramenti.
Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads