Lugha za Kiberiberi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Lugha za Kiberiberi
Remove ads

Lugha za Kiberiberi au Kiamazighi ni kundi la lugha za Kiafrika-Kiasia zinazosemwa hasa Moroko na Aljeria lakini pia kati ya wakazi wa jangwa kubwa la Sahara hadi eneo la Sahel. Ni lugha ya Waberiberi wanaoishi kati ya wasemaji wa Kiarabu katika Afrika ya Kaskazini.

Thumb

Aina za Tamazight au lugha za Kiberiberi katika Afrika ya Mashariki.

         Kitwareg          Kizayani
         Kirifi          Kishanawa
         Kikabile          Kishawia
         Kishilha          Kiberiberi cha Sahara
Thumb
Alama ya barabarani ya "Stop!" kwa Kiarabu na Kitamazight nchini Moroko.
Remove ads

Historia

Wasemaji wa Kiberiberi wanatazamwa kuwa ndio wakazi asilia wa Afrika ya Kaskazini kabla ya kuja kwa Waroma wa Kale na Waarabu. Tangu uenezi wa Kiarabu matumizi ya Kiberiberi yamerudi nyuma polepole. Wakazi wengi wa nchi za Afrika ya Kaskazini ni wa asili ya Kiberiberi lakini kwa kawaida kupotea kwa lugha humaanisha pia upotevu wa tabia ya kuwa Mberiberi. Leo hii wamebaki wasemaji milioni 10 na wengi wao hutumia lugha yao pamoja na Kiarabu au Kifaransa katika maisha ya kila siku.

Utambuzi wa lugha za Kiberiberi umeongezeka katika karne ya 21, huku Moroko na Algeria zikiongeza Tamazight kama lugha rasmi kwa katiba zao mwaka wa 2011 na 2016 mtawalia.

Remove ads

Mwandiko

Kiberiberi kimeandikwa tangu miaka elfu kadhaa. Mifano ya kale kabisa imehifadhiwa tangu 200 KK iliyoandikwa kwa mwandiko wa Tifinagh unaoendelea kutumiwa na Watuareg. Aina hiyo imekuwa mwandiko rasmi nchini Moroko tangu mwaka 2003 pamoja na ule wa Kiarabu na ule wa Kilatini.

Tangu mwaka 1000 na uenezi wa Uislamu lugha imeanza kuandikwa kwa alfabeti ya Kiarabu.

Katika karne ya 20 imeandikwa mara nyingi kwa mwandiko wa Kilatini, na katika nchi nyingi zilizokuwa makoloni ya Ufaransa mwandiko ni Kilatini hadi leo.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha za Kiberiberi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads