Ushanga wa sala
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ushanga wa sala ni ushanga uliotengeneza kwa ajili ya kusali kwa kukariri maneno kadhaa ya imani.

Shanga zilitumika kama pambo tangu kale: barani Afrika zimepatikana za miaka 10,000 KK.
Lini na wapi zilianza kutumika kwa ajili ya sala haijulikani, lakini kuna sanamu ya karne ya 3 KK inayomuonyesha Mhindu akiwa na ushanga wa sala.
Lengo ni kutunza hesabu ya kauli ambazo zinakaririwa kwa kupitisha vidole viwili juu ya punje zilizounganishwa katika kamba au uzi kama kwa Wakristo Waorthodoksi (kamba ya sala) na Wakatoliki (rozari).
Remove ads
Picha za Kikristo
- Komboskini ya mafundo 100 kwa Waorthodoksi Wagiriki.
- "Lestovka" ya ngozi kwa Waorthodoksi Warusi.
- Rozari ya Bikira Maria kwa Wakatoliki.
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads