Wakfu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wakfu
Remove ads

Wakfu (kwa Kiarabu وقف‎‎) inamaanisha hali ya kutengwa na matumizi mengine, hasa kwa ajili ya matumizi ya kidini au manufaa kwa umma tu.

Thumb
Mtakatifu Genevieve akiwekwa wakfu na askofu: mchoro wa mwaka 1821 (Ste. Genevieve, Missouri).

Watu, vitu na mahali wanaweza kuwekwa wakfu kwa namna mbalimbali.

Maana ya Kisheria

Kwa maana ya kisheria wakfu (kwa Kiingereza foundation au charitable trust) ni taasisi au shirika lililopokea mali au pesa kwa matumizi ya manufaa kwa umma.

Sheria za Kenya[1] zinaruhusu mali kuwekwa wakfu kwa manufaa ya dini, elimu, utamaduni, sayansi, jamii, michezo au usaidizi wa watu maskini[2].

Mali ya taasisi ya aina hiyo imo mikononi mwa wadhamini (ing. trustees) wenye wajibu wa kutunza mali ya wakfu kwa madhumuni yaliyoelezwa katika hati ya taasisi na kuandikishwa katika ofisi ya serikali.

Kimsingi taasisi ya wakfu ilipokea mali ambayo ni msingi wa kazi yake, kwa mfano ardhi, majengo, hisa au pesa. Kuna pia mifano ya taasisi za wakfu zisizo na rasilmali zikitafuta zaidi michango ya wafadhili kwa ajili ya kazi yao kulingana na madhumuni. [3]

Remove ads

Ukristo

Katika Ukristo, watu wanaweza kuwekwa wakfu, hasa kwa njia ya sakramenti zisizoweza kurudiwa kwa sababu zinatia alama isiyofutika milele (yaani ubatizo, na kwa madhehebu mengine pia kipaimara na daraja takatifu), lakini pia kwa kushika maisha ya pekee katika useja mtakatifu (kwa kawaida pamoja na ufukara na utiifu).

Vitu na mahali vinaweza kuwekwa wakfu hasa kwa ajili ya ibada, k.mf. vyombo vya ibada, mavazi ya ibada na kanisa.

Remove ads

Uislamu

Katika Uislamu wakfu ni mali iliyotengwa kwa kusudi la kidini. Mifano ya wakfu ni kutoa kiwanja kwa kujenga msikiti, shamba au nyumba ikiwa mapato yake yatagharamia misikiti, madrasa, hospitali, watu maskini au wanafunzi, au pia kutoa pesa kwa makusudi haya.

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads