Valentinus
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Valentinus (Terni, Italia, 176 hivi - Roma, 14 Februari 273) alikuwa askofu wa Terni.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini katika Kanisa Katoliki, lakini pia na Waorthodoksi, Waanglikana na Walutheri kadhaa.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Februari ya kila mwaka[1].
Valentinus anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa kote duniani kama Valentine's Day.
Remove ads
Historia
Historia yake inawezekana inamchanganya na Valentinus mwingine, padri wa karne ya 3 huko Roma, aliyeuawa mwaka 269 katika mazingira yaleyale [2].
Hadithi
Kuna hadithi mbalimbali juu yake. Mojawapo inasema Valentinus aliandika barua kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa maneno haya: Kutoka kwa Valentinus wako.
Mbali ya hadithi, askofu huyo alijulikana kwa miujiza yake. Huko Terni, mnamo 2011, ilipatikana mifupa ya Sabino e Serapia: mmoja alikuwa Mpagani akida wa jeshi la Roma, mwingine msichana Mkristo motomoto. Kwa ajili yake Sabino aliongokea Ukristo, lakini baada ya muda mfupi aligundua kwamba Serapia ni mgonjwa wa kifua kikuu. Ili asitengane naye, Sabino alimuomba Valentinus, naye alibariki ndoa yao na kuomba mapendo yao yadumu milele. Baadaye walifariki pamoja wamekumbatiana na ndivyo mifupa yao inavyopatikana hadi leo.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads