Waberiberi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Waberiberi
Remove ads

Waberiberi ni wakazi asilia wa Afrika ya Kaskazini kuanzia Moroko hadi Misri na nchi za Sahara. Wenyewe wanajiita Amazigh (au: Imazighen) yaani "watu huru".

Thumb
Maeneo yenye wasemaji wa lugha za Kiberiberi (Tamazight).

Kabila lao mojawapo linalojulikana hasa ni Watuareg wanaokalia maeneo ya jangwa kubwa la Sahara.

Leo hii wamepungua kwa sababu wengi wamezoea kutumia lugha ya Kiarabu, hivyo wanahesabiwa kati ya Waarabu.

Wanaoendelea kutumia lugha ya Kiberiberi kama lugha ya kwanza ni:

Katika nchi kavu jangwani au karibu na jangwa maisha yao ni ya ufugaji na kuhamahama. Mlimani wanalima. Leo hii ni hasa Watuareg wanaoendelea na maisha ya kuhamahama.

Remove ads

Historia

Katika historia wamejulikana tangu ilipoanza kuandikwa. Waroma na Wagiriki wa Kale waliwaita kwa majina kama Wanumidia, Wagaramanti au Walibya.

Kabla ya unenezaji wa Uislamu wengi walikuwa Wakristo na mashuhuri kati hao alikuwa Monika, mama wa Agostino wa Hippo.

Mberiberi anayejulikana sana leo ni mchezaji wa mpira wa Ufaransa Zinédine Zidane.

Viungo vya nje

Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads