Tunisia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Tunisia, rasmi kama Jamhuri ya Tunisia (kwa Kiarabu الجمهرية التونسية, al-Jumhūrīya at-Tūnisīya), ni nchi katika Afrika Kaskazini, inayopakana na Bahari ya Mediteranea kaskazini na mashariki, Aljeria magharibi, na Libya kusini-mashariki. Ina idadi ya watu takriban milioni 12, ikiwa ya 79 duniani. Jiji lake kubwa zaidi ni Tunis, ambalo pia ni mji mkuu. Tunisia imegawanyika katika majimbo 24 yanayosimamia utawala wa ndani. Inajulikana kwa makazi ya ustaarabu wa Karthago.
Remove ads
Historia
Tunisia iliwahi kutawaliwa na Wafinikia walioanzisha huko mji wa Karthago.
Baada ya hao kushindwa na Roma ya Kale, ilikuwa jimbo la Afrika katika Dola la Roma.
Kisha eneo lake likatawaliwa kwa awamu na Wavandali, Waarabu, Wahispania, Waturuki na Wafaransa.
Mnamo tarehe 20 Machi 1956 Tunisia ilipewa uhuru wake kutoka kwa Wafaransa.
Watu
Wakazi karibu wote (98%) wanajiita Waarabu na hutumia lugha ya Kiarabu ambacho ndicho lugha rasmi. Hata hivyo damu yao ni mchanganyiko hasa wa ile ya Waberber, Waarabu na Waturuki.
Takriban watu 200,000, hasa kusini, wanaendelea kuzungumza Kiberber ambacho ni lugha asili ya wenyeji lakini Waberber wengi wamezoea kutumia Kiarabu.
Katika elimu na biashara Kifaransa kinatumika pia sana.
Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na asilimia 99 za wakazi, nao ndio dini rasmi, lakini theluthi moja kati yao, na nusu kati ya vijana, wanajitambulisha kama wasio na dini, kiwango kikubwa kuliko nchi zote za Kiarabu. Waliobaki ni Wakristo, hasa Wakatoliki, na Wayahudi wachache.
Remove ads
Tazama pia
Viungo vya nje
- Government of Tunisia (official website).
- Tunisia entry at The World Factbook
- Tunisia katika Open Directory Project
- Tunisia profile from BBC News.
- Wikimedia Atlas of Tunisia
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Tunisia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads