Monika
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Monika (Tagaste, Numidia, leo Algeria 332 - Ostia, kitongoji cha Roma, Italia, 387) alikuwa mwanamke wa kabila la Kiafrika la Waberberi ambaye aliolewa mapema na Patricius, afisa wa Dola la Roma, akamzalia watoto, mmojawao Agostino wa Hippo[1].

Kwa ajili ya uongofu wake alisali sana na kutoa machozi mengi mbele ya Mungu hadi akasikilizwa. Ndipo alipopotewa na hamu ya kuishi akatamani tu kwenda mbinguni akafariki dunia kabla hajarudi Afrika [2].
Ni maarufu hasa kutokana na sifa alizomwagiwa mwanae huyo katika kitabu cha Maungamo (Confessiones).
Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu, hasa tarehe 27 Agosti[3] au 4 Mei.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads