Waherero
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Waherero ni kabila la watu wa jamii ya Wabantu wanaoishi hasa nchini Namibia, na pia sehemu za Botswana na Angola.[1]
Lugha yao kuu ni Kiherero, ambayo ni sehemu ya kundi la Lugha za Kibantu. Watu wa jamii ya kabila hili hujishughulisha zaidi na ufugaji wa mifugo kama ng’ombe na mbuzi, ambapo ni alama muhimu ya utamaduni wao.
Historia
Katika historia, Waherero walikumbwa na mauaji ya kimbari kati ya miaka ya 1904 na 1908, wakati wa ukoloni wa Kijerumani nchini Namibia, ambapo maelfu waliuawa au kufa kutokana na njaa na mateso. Hadi sasa Waherero wanaendelea kudumisha mila zao, pamoja na mavazi ya pekee yenye asili ya Ulaya ya karne ya 19 ambayo yalibadilishwa kulingana na tamaduni zao.[2]
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads