Ujanseni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ujanseni ulikuwa tapo la teolojia ya Kanisa Katoliki (hasa nchini Ufaransa) katika karne ya 17 na ya 18. Tapo hilo lilisisitiza dhambi ya asili, uovu wa binadamu uliosababishwa nayo, haja ya neema ya Mungu na uteule kwa kudai linafuata mafundisho ya Augustino wa Hippo.

Tapo lilitokana na vitabu vya mwanateolojia wa Uholanzi Cornelius Jansen vilivyochapishwa baada ya kifo chake (1638). Rafiki yake, abati Jean Duvergier de Hauranne, alisambaza mafundisho yake kwanza, na alipokufa yeye pia (1643) juhudi ziliendelezwa na Antoine Arnauld, lakini pia na Pierre Nicole, Blaise Pascal na Jean Racine.
Ujanseni ulipingwa na wengi, hasa Wajesuiti, kwa kuona unafanana na Ukalvini.[1]
Mwaka 1653, kwa hati Cum occasione, Papa Innocent X alilaani kama uzushi kauli tano za Wajanseni.[1] Viongozi wao walijaribu kulegeza msimamo wao bila kuachana nao kabisa, lakini hatimaye walihukumiwa tena na hati Unigenitus Dei Filius ya Papa Klementi XI mwaka 1713.[2]
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads