Wamormoni

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wamormoni
Remove ads

Wamormoni ni kundi la watu wanaohusiana na dini ya Mormoni, iliyoanzishwa na Joseph Smith huko New York, Marekani, katika miaka ya 1820 akidai alipata njozi na kuonyeshwa kitabu kitakatifu.

Thumb
Kioo cha rangi kikionyesha njozi ya kwanza ya Joseph Smith.

Baada ya kifo chake (1844), Wamormoni walimfuata Brigham Young hadi eneo la Utah.

Leo wengi wao ni waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku ya Mwisho (kifupisho cha Kiingereza LDS Church).

Kiini cha utamaduni wao ni jimbo la Utah, ambapo wao ndio wengi kati ya wakazi wote, lakini siku hizi Wamormoni wanaoishi nchini Marekani ni wachache kuliko wanaoishi nje kutokana na umisionari mkubwa wanaoufanya duniani kote.

Idadi yao inakadiriwa kuwa milioni 15.

Remove ads

Imani yao

Thumb
Mpango wa Wokovu.

Wamormoni wanasadiki Biblia pamoja na maandishi mengine kama vile Kitabu cha Mormoni.

Wanasisitiza sharti la kumfuata Yesu Kristo ili kumrudia Mungu, pamoja na kupata ubatizo.

Wamormoni wanajiita Wakristo, ingawa mafundisho yao mbalimbali ni tofauti na yale ya madhehebu yote ya Ukristo, kiasi cha kutokubaliwa nayo (k.mf. Kanisa Katoliki halitambui ubatizo wao, hivyo linawahesabu kama dini tofauti).

Remove ads

Maadili

Wamormoni wana maadili imara upande wa jinsia (wakipinga uasherati, uzinifu na ushoga) na wa matumizi ya mwili (vileo, tumbaku, kahawa, chai n.k.).

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads