Wapaskwali
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wapaskwali (jina rasmi: Wakonventuali Wareformati) walikuwa tawi la Hispania la utawa wa Ndugu Wadogo lililotokana na juhudi za kuleta urekebisho za Yohane Pascual (karne ya 15 - 1553). Ndiyo sababu waliitwa hivyo. Juhudi hizo zilifuata zile za namna hiyo za Yohane wa Puebla (1453 - 1495) na Yohane wa Guadalupe (karne ya 15 - 1506), ambaye wafuasi wake walitangulia kuitwa Wakonventuali Wareformati wakajulikana zaidi kama Waguadalupe.
Hatimaye Petro wa Alkantara (1499 - 1562) alihamia kanda yao na kuistawisha hata tawi likaitwa la Waalkantara au Ndugu Wadogo Pekupeku.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads