Wareformati
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wareformati ni jina la watawa wa mashirika mbalimbali waliofuata urekebisho (kwa Kiingereza: "reform"). Ndiyo sababu waliitwa Wareformati.
Wafransisko Wareformati

Kwa mfano, katika karne ya 16 Ndugu Wadogo wa Italia waliokuwa hawajajiunga na Wakapuchini lakini walipenda maisha magumu zaidi kadiri ya kanuni ya Fransisko wa Asizi waliruhusiwa kuenda kuishi pamoja katika konventi za urekebisho.
Ndugu waliojikusanya katika makao ya upwekeni kuanzia mwaka 1535 (mkutano mkuu wa shirika ulipowaruhusu ili kuzuia wengine wengi wasiwakimbilie Wakapuchini [1]), kisha kuongezeka waliwekwa moja kwa moja chini ya Mtumishi mkuu tu (1579), wakapewa katiba maalumu (1595), ruhusa za pekee sana (1596), hatimaye Kiongozi mkuu na mkutano mkuu wa kwao. Hivyo mamlaka ya Mtumishi wa OFM kwao ikawa jina tu.
Mwaka 1762 Wareformati walifikia kuwa 19.000 hivi.[2]
Kati yao hadi kipindi hicho tunawakuta watakatifu mabradha watatu: Benedikto Mwafrika (+1589), mtoto wa watumwa huko Italia, Mwafrika wa kwanza kutangazwa mtakatifu, Umile wa Bisignano (+1637), mnyenyekevu ajabu, na Karolo wa Sezze (+1670), aliyeandika vizuri sana kuhusu maisha ya kiroho; halafu mapadri Pasifiko wa San Severino (+1721), aliyezingatia sana maisha ya sala, na Leonardo wa Portomaurizio (+1751), tunda bora la Kirekebisho kilichoanzia mjini Roma karne ya 17. Pia walipatikana wenye heri 4.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads