Warombo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Warombo ni watu wa mkoa wa Kilimanjaro, jamii ya Wachagga.

Lugha zao ni Kiseri na lahaja nyingine za Kichagga, yenye asili ya Kibantu[1]. Warombo wameenea mkoa wote na hutambuana kwa kuelewana katika mazungumzo.

Warombo wanajishugulisha na kilimo, ufugaji, biashara na kazi za ofisini.

Vyakula na vinywaji

Chakula asili cha Warombo ni kitheri, umberere, mabande, ngolowo, irombwe, ng'ande na mtori. Hata hivyo kwa sasa mtori unaliwa na watu mbalimbali ambao si Wachagga na hupikwa hotelini kama chakula.

Kinywaji cha asili cha Warombo kinaitwa Busa. Hapo zamani Warombo walikuwa wanakunywa busa kipindi wakifanya matambiko mbalimbali, kwani ni kinywaji mahususi kinachotayarishwa ili kitumike wakati wa tambiko. Matambiko ya Warombo hufanyika wakati wowote katika mwaka, pia hufanyika kwa lengo la kumwomba Mungu awasaidie katika mambo mbalimbali. Tambiko hufanyika katika mti maalumu ulioandaliwa kwa ajili hiyo na huoteshwa katika kila kaya kwa ajili ya kutunza mazigira na chakula cha mifugo.

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads