Mtori

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mtori
Remove ads

Mtori ni chakula ambacho kinapendwa na Wachagga wengi nao hupenda kukila hasa wakati wa usiku. ingawa leo mijini wengi hupendelea kula wakati wa asubuhi zaidi. Na vilevile ni chakula cha wagonjwa, hasa wale wasioweza kula chakula kigumu. Chakula hiki cha mtori kina asili ya Arusha, Tanzania.[1][2]

Thumb
Mtori

Matayarisho ya Mtori

  • Ndizi laini au ndizi ng'ombe
  • Nyama hasa ya utumbo
  • Sowe (inatokana na viazi vyenye asili ya magimbi) au viazi mviringo
  • Vitunguu
  • Supu ya nyama
  • Chumvi

Utengenezaji

Nyama hupikwa mpaka kuwa laini na pia kupata supu ambayo itatumika wakati wa kuponda ndizi. Pia ndizi hupikwa pamoja na vitunguu na nyanya mpaka kuwa laini kabisa. Baada ya hapo maji yakikauka ndizi hizo hupondwa pondwa mpaka kuwa kama ugali. Sasa supu iliyobaki kwenye nyama inachanganywa na ndizi zilizopondwa mpaka kupata kitu kama uji ambao ni mtori, tayari kwa matumizi hasahasa ikiwa bado moto.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads