Warshawa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Warshawa
Remove ads

Warshawa (kwa Kipoland: Warszawa; kwa Kiingereza Warsaw) ni mji mkuu wa Poland pia mji mkubwa wa nchi, wenye wakazi milioni mbili hivi (1.78 mln - 2018).

Ukweli wa haraka Nchi, - Wakazi kwa ujumla ...
Remove ads

Jiografia

Warshawa iko katikati ya bonde la mto Vistula (Kipoland: polnisch Wisła, takriban km 350 kutoka Bahari Baltiki.

Historia

Warshawa imekuwa mji tangu karne ya 13, ikawa mji mkuu wa Poland mwaka 1596.

Iliharibiwa mara nyingi katika historia yake, hasa wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Wapoland walijaribu kuasi dhidi ya Wajerumani walioshika mji kati ya miaka 1939 na 1944; pamoja na vifo vingi, asilimia 90 za nyumba zote ziliharibiwa.

Baada ya vita mji ulijengwa upya mara nyingi kwa kurudisha nyumba zinazofanana na nyumba za kale.

Kitovu chake kimeorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.

Remove ads

Utamaduni

Kuna vyuo 66 pamoja na Chuo Kikuu cha Warshawa, vyuo vikuu vingine, nyumba za maigizo, opera na makumbusho mbalimbali.

Uchumi

Warshawa ni mji wa viwanda vingi vya kutengenezea chuma, mashine, motokaa na mengine mengi.

Picha za Warshawa

Tazama pia

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Poland bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Warshawa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads