Waslavi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Waslavi (kwa Kiingereza Slavs, pia "Slavic" au "Slavonic people") ni kundi kubwa la mataifa yanayotumia lugha za Kihindi-Kiulaya barani Ulaya. Pamoja na kuwa wenyeji wa nchi za Ulaya Mashariki, Ulaya ya Kati na Ulaya Kusini kuanzia karne ya 6 BK, tangu zamani wameenea Asia Kaskazini na Asia ya Kati. Nchi zao zinatawala zaidi ya 50% za bara la Ulaya.


Remove ads
Tofauti
Wanagawanyika kati ya Waslavi wa Magharibi (hasa Wapolandi, Wacheki na Waslovaki), Waslavi wa Mashariki (hasa Warusi, Wabelarus na Waukraina), na Waslavi wa Kusini (hasa Waserbi, Wakroati, Wabosnia, Wamakedonia, Wasloveni, Wamontenegro na Wabulgaria).
Mahusiano yao yanatofuatiana, kuanzia hisia ya kuwa na mengi ya pamoja hadi kuchukiana kabisa na kupigana vita kwa ukatili.[1]
Idadi
Duniani kote Waslavi wanakadiriwa kuwa milioni 360. Kati yao wanaongoza Warusi, Wapolandi na Waukraina.
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads