Yael Abecassis
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yael Abecassis (Kiyahudi: יעל אבקסיס ; amezaliwa Ashkelon, Israeli, 19 Julai 1967) ni mwigizaji filamu na mwanamitindo kutoka nchini Israeli.
Wasifu
Yael Abecassis alizaliwa na Wayahudi kutoka Moroko. Ni binti Raymonde Abecassis, mwigizaji na mwimbaji wa Israel.[1]
Abecassis alioana na mwigizaji wa Israel Lior Miller mwaka 1996 na kujaliwa mtoto mmoja. Walitalakiana mwaka 2003. Kwa sasa ameolewa na mjasiriamali Ronny Douek.
Kazi ya uigizaji na mitindo
Yael Abecassis alianza uanamitindo akiwa na umri wa miaka 14. Baadae alijikita katika runinga na filamu, akionekana katika matangazo na kuwa mhusika mkuu aliyetambulika kwa jina la Rivka katika filamu ya Kadosh. Ni filamu ya mwaka 1999 ikiongzwa na Amos Gitai. Katika miaka ya tisini, alikuwa mtayarishaji wa vipindi vya watoto katika runinga ya Israel na kutayarisha video za muziki kwa watoto. Mwishoni mwa miaka ya 1990, aliacha kazi ya runinga na kujihusisha na uigizaji.
Remove ads
Filamu alizoigiza
- Hunting Elephants (2013), Dorit
- Prisoners of War (2010), Talia Klein
- Shiva (2008), Lili
- Survivre avec les loups (2007)
- Sans moi (2007), Marie
- Papa (2005/II), Léa
- Va, vis et deviens (2005), Yaël Harrari
- Until Tomorrow Comes (2004), Daughter
- Alila (2003), Gabi
- Ballo a tre passi (2003)
- Haïm Ze Haïm (2003)
- Miss Entebbe (2003), Elise
- Bella ciao (2001), Nella
- Maria, figlia del suo figlio (2000), Mary of Nazareth
- Kadosh (1999), Rivka
- Shabatot VeHagim (1999), Ella
- Passeur d'enfants (1997), Yael
- L'enfant de la terre promise (1997), Yael
- L'enfant d'Israel (1997)
- Hakita Hameofefet (1995)
- Ha-Yerusha (1993)
- Zarim Balayla (1993)
- Sipurei Tel-Aviv (1992), Sharona
- Pour Sacha (1991), Judith
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads