Yehoramu wa Yuda
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yehoramu wa Yuda (kwa Kiebrania: יְהֹורָם, Yəhōrām, yaani Yahweh ametukuka; pia: יוֹרָם Yōrām; 882 KK hivi - 842 KK hivi) alitawala ufalme wa Yuda kati ya miaka 849 KK na 842 KK baada ya kuua ndugu zake 6.

Kwa kuoa Atalia, binti Ahabu, alifuata sera za ufalme wa Israeli dhidi ya Mungu pekee, YHWH, kinyume na alivyofanya baba yake Yehoshafati. Biblia inaeleza ndiyo sababu ya kushindwa kutawala kwa mafanikio.
Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 8 na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 21-22.
Pia anatajwa na Injili ya Mathayo kati ya mababu wa Yesu Kristo.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
