Atalia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Atalia (kwa Kiebrania: עֲתַלְיָה, ʻĂṯalyâ, "Mungu anainuliwa"[1]) alikuwa malkia wa ufalme wa Yuda kama mke wa mfalme Yehoramu wa Yuda, aliyekuwa wa ukoo wa Daudi.


Baada ya mume wake kufa, Atalia alijitwalia madaraka kinyume cha taratibu na kwa ukatili mkubwa (2Fal 11:1)[2] akatawala miaka 841–835 KK, mpaka alipopinduliwa na kuuawa (2Fal 11:14-16; 2Nya 23:12-15).
Binti au dada wa mfalme Ahabu wa Israeli, alijitahidi kueneza ibada kwa Baali na miungu mingine dhidi ya YHWH, Mungu pekee wa dini ya Musa.
Baada yake alitawala mjukuu wake, Yehoashi, mrithi halali wa mfalme Ahazia wa ukoo wa Daudi. Ni kwamba Atalia alipoua wajukuu wake wote ili kuteka nchi, Yehosheba, dada wa Ahazia, alifaulu kumuokoa mtoto wake wa mwaka mmoja, Yehoashi, akamlea kwa siri hekaluni akishirikiana na mumewe, kuhani Yehoyada, hata akaweza kumtawaza katika kiti cha enzi cha babu yao Daudi].
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
