Yese

From Wikipedia, the free encyclopedia

Yese
Remove ads

Yese au Yishai (kwa Kiebrania: יִשַׁי, Yišay, Yīšáy, maana yake "Mfalme" au "Mungu yupo" au "Zawadi ya Mungu"; kwa Kigiriki: Ἰεσσαί, Iessai; kwa Kilatini: Isai, Jesse) ni mtu anayetajwa na Biblia kama baba wa mfalme Daudi wa Israeli. Huyu pengine anatajwa tu kama "Mwana wa Yese" (Ben Yishai). Hivyo anatajwa pia katika orodha ya vizazi vya Yesu (Math 1:1-17).

Thumb
Yesse katika kioo cha rangi, All Saints Church, Hove, Sussex, Uingereza.

Baba yake alikuwa Obedi, mwana wa Boazi na Ruthu. Kama hao wote aliishi Bethlehemu.

Mtu wa kabila la Yuda, alizaa watoto saba wa kiume, Daudi akiwa wa mwisho wao.[1] Kitabu cha Kwanza cha Mambo ya Nyakati kinawataja hivi: Eliabu, Abinadabu, Shimea, Nethaneli, Raddai, Ozem na Daudi mbali ya mabinti wawili, Zeruia and Abigaili.[2]

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads