Yosefu Manyanet

From Wikipedia, the free encyclopedia

Yosefu Manyanet
Remove ads

Yosefu Manyanet (jina kamili: Josep Manyanet i Vives; Tremp, Lleida, 7 Februari 1833 – San Andreu del Palomar, Barcelona, 17 Desemba 1901) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Hispania.

Thumb
Mt. Yosesu Manyanet.

Baada ya kuwa paroko sehemu mbalimbali, alianzisha shirika la Wana wa Familia Takatifu, pamoja na lile ya Mabinti Wamisionari wa Familia Takatifu ili kusaidia familia zote kuwa bora kwa kufuata mfano wa ile takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu.[1][2][3]

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 25 Novemba 1984 halafu mtakatifu tarehe 16 Mei 2004.[4]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[5].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Machapisho yake

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads