Mzeituni

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mzeituni
Remove ads

Mzeituni au mzaituni (jina la kisayansi kwa Kilatini Olea europaea, yaani "mzeituni wa Ulaya", au Olea sylvestris, yaani "mzeituni mwitu") ni mti mfupi wa familia ya Oleaceae unaopatikana hasa kandokando ya Bahari ya Kati, lakini pia sehemu nyingine za Afrika na Asia.[1]

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Matunda yake (zeituni au zaituni) ni muhimu hasa kwa utengenezaji wa mafuta (90%), ingawa yanaliwa pia bila kushindiliwa (10%).

Inaonekana asili ya ulimaji wake ni Uajemi na Mesopotamia miaka 6,000-7,000 iliyopita. Kutoka huko ulienezwa sehemu nyingine.

Leo uzalishaji ni mkubwa hasa Hispania, halafu Italia, Ugiriki, Uturuki n.k.

Mbali ya faida hiyo, toka zamani tawi la mti huo linatazamwa kama ishara ya wingi, utukufu na amani. Kwa sababu hiyo lilitolewa kwa miungu na kwa washindi.

Remove ads

Picha

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads