Zebedayo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Zebedayo
Remove ads

Zebedayo (kwa Kigiriki Ζεβεδαῖος, Zebedaios, kutoka Kiebrania זְבַדְיָה, Zvad'yah[1], yaani Mwingi au Zawadi yangu[2]), kadiri ya Injili zote nne, alikuwa baba wa Mitume wawili wa Yesu Kristo: Yakobo Mkubwa na Yohane.

Thumb
Mchoro wa Hans von Kulmbach, Maria Salome na Zebedayo pamoja na wanao Yakobo Mkubwa na Yohane Mwinjili, 1511 hivi.

Injili zinamtaja pia mke wake, Salome[3], ambaye pia alifuatana na Yesu hadi kifo chake msalabani huko Kalivari, nje kidogo ya ngome ya Yerusalemu.

Zebedayo aliishi kwenye Ziwa Galilaya[4] na kuwa mvuvi mwenye wafanyakazi chini yake (Mk 1:19-20; Math 4:21-22; Lk 5:4)[4][5]

Injili zinamtaja pia katika mistari mingine: Math 10:2; 20:20; 26:37; 27:56; Mk 3:17; 10:35; Lk 5:10 na Yoh 21:2.

Baadhi ya wataalamu wanadhani alikuwa pia kuhani.

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads