From Wikipedia, the free encyclopedia
Bahari Kuu (ing. w:ocean) ni jina linalotumika kutaja jumla ya maeneo makubwa ya maji ya chumvi duniani yanayopakana na kufuatana kama gimba moja. Kwa maana hii bahari kuu inafunika zaidi ya theluthi mbili za uso wa dunia.
Bahari Kuu imegawiwa na ardhi ya mabara kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia lakini sehemu zake zinaungana kwenye nusutufe ya kusini.
Eneo hili kubwa huhesabiwa mara nyingi kama bahari kuu tatu yaani:
Hizi sehemu tatu hutajwa pia kama "bahari kuu" kwa kuzitofautisha na maeneo madogo zaidi ya maji ya chumvi au sehemu zinazoitwa bahari ya kando. [1]
Wakati mwingine Bahari ya Aktiki na Bahari ya Antaktiki hutajwa kama bahari kuu ("oceans") za pekee.
Bahari kuu hushika asilimia 97% ya maji yote duniani. Hadi sasa ni asilimia 5 pekee zilizofanyiwa utafiti kamili. [2] Kiasi cha maji yote kwenye bahari kuu ni takriban kilomita za mjazo bilioni 1.3.
Kiasi cha maji baharini kinajulikana kuwa kilicheza na kubadilika katika historia ya dunia. Wakati wa vipindi vya baridi duniani, kama vile enzi ya barafu, sehemu kubwa ya maji yalipatikana kwa umbo la barafu na maji kiowevu yalikuwa kidogo. [3]. Kuongezeka kwa halijoto duniani kunasababisha kupanda kwa uwiano wa bahari kote duniani. Nchi mbalimbali hasa kwenye pwani au nchi za visiwa zitapungua kieneo.
Halijoto ya bahari na mikondo yake ni athira muhimu mno kwa ajili ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.